Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, hafla hiyo iliwakutanisha waumini na wanajumuiya kutoka sehemu mbalimbali za jamii ya Kiislamu kwa ajili ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.), ambaye maisha yake matukufu yameendelea kuwa mwongozo kwa wanadamu katika nyanja mbalimbali za maisha.
Katika maadhimisho hayo, washiriki walikumbushwa umuhimu wa kujifunza kutoka katika tabia njema, mwenendo bora na mafundisho ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.), huku wakisisitiziwa ujumbe wake wa kudumu unaohimiza rehema, umoja, upendo na uongofu wa Mwenyezi Mungu.
Maulidi hayo pia yalitoa fursa ya kuhuisha mafundisho na mwenendo wa Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) miongoni mwa jamii, hususan katika kipindi ambacho umoja, mshikamano na maadili mema yanahitajika katika kujenga jamii yenye amani na kuheshimiana.
Kupitia hafla hiyo, Jumuiya ya Ahlulbay (as) ABAK, kwa kushirikiana na taasisi hizo, imeendelea kutoa nafasi kwenye jamii ya kukutana, kukumbuka historia tukufu ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na kutafakari ujumbe wake wa rehema, umoja na uongofu wa Mwenyezi Mungu.




Maoni yako